Ujenzi wa mahandaki ya kuhifadhi taka za nyuklia kwa maelfu ya miaka - BBC News Swahili (2024)

Ujenzi wa mahandaki ya kuhifadhi taka za nyuklia kwa maelfu ya miaka - BBC News Swahili (1)

Chanzo cha picha, Tapani Karjanlahti/ TVO

Taka za nyuklia hubaki kuwa sumu kwa maelfu ya miaka.

Futi 1,500 (450m) chini ya vilima vya eneo la Champagne kaskazini mashariki mwa Ufaransa, kuna eneo lililochongwa kwenye mwamba kama mahali pa kuzikia baadhi taka za nyuklia.

Kufika huko utaendesha gari kwa saa nne kutokea mashariki mwa Paris, na kuna kilomita 2.4 (maili 1.5) za mahandaki ambayo ni maeneo ya majaribio ya kisayansi ya mbinu za ujenzi na ubunifu wa kiteknolojia katika kuhifadhi sumu hizo.

Pia unaweza kusoma

Ujenzi wa mahandaki ya kuhifadhi taka za nyuklia kwa maelfu ya miaka - BBC News Swahili (2)

Chanzo cha picha, Tapani Karjanlahti/TVO

Finland ilikuwa nchi ya kwanza duniani kujenga kituo kirefu cha chini ya ardhi cha utupaji wa taka ya nyuklia za mafuta yaliyotumika, na sasa imeingia katika hatua ya kwanza ya majaribio ya uwekaji wa taka hizo.

Nchini Sweden, ujenzi unakaribia kuanza, ni mwendo wa saa mbili kwa gari kaskazini mwa Stockholm, na kituo kama hicho kinatarajiwa kujengwa nchini Ufaransa hivi karibuni.

Nchini Uingereza eneo litakalojengwa hifadhi kama hiyo bado halijachaguliwa.

Mahandaki hayo ni makubwa, ghali na yenye utata yanayoundwa kuhifadhi taka nyingi za mionzi na kwa muda mrefu zinazozalishwa na nyuklia.

Kwa sasa, taka hizi zimehifadhiwa juu ya uso wa dunia katika vituo kama kile cha Sellafield nchini Uingereza, na La Hague nchini Ufaransa. Uchafu huo unaweza kujumuisha vifaa vya vinu vya nyuklia, kaboni kutoka katika kinu, mafuta na maji maji kutoka katika mafuta yaliyotumika kutoka vinu vya nyuklia.

Changamoto za uhifadhi

Ujenzi wa mahandaki ya kuhifadhi taka za nyuklia kwa maelfu ya miaka - BBC News Swahili (3)

Chanzo cha picha, Andra

Kupata maeneo ambayo yataendana na mahitaji ya kuhifadhi taka hizi pia ni changamoto. Hasa ikiwa eneo linalofaa liko kwenye jamii inayoishi watu.

"Utoaji leseni kwa vituo hivi vya utupaji taka huchukua zaidi ya miaka 20 hadi 30," anasema Jacques Delay, mwanasayansi katika kituo hicho nchini Ufaransa, "na kutupa taka kutadumu kwa takriban miaka 100 kabla ya kufungwa." Baada ya hapo, kutakuwa na mamia ya miaka ya ufuatiliaji wa eneo hilo.

Wataalamu huchunguza ikiwa eneo lina miamba ya chini ya ardhi ya karibu mita 500 hadi kilomita 1 na yanafaa kuweka taka za nyuklia kwa zaidi ya miaka 100,000.

Nchini Finland "tumekuwa tukitengeneza umeme wa nyuklia tangu mwishoni mwa miaka ya 70," anasema Pasi Tuohimaa wa Posiva Oy, kampuni ya utupaji taka za nyuklia ya Finland.

Migodi ya madini haikujengwa kwa usahihi unaohitajika ili kuhifadhi taka za kiwango cha nyuklia. Na ikiwa taka hizo zitawekwa huko na bado kuna rasilimali za madini hatari ya watu kuendelea na uchimbaji ni kubwa.

Pia kuwa rahisi zaidi kujenga kituo kipya kinachojengwa kwa madhumuni ya taka za nyuklia. Kujenga kituo kipya huruhusu kupanga eneo zima kuanzia mwanzo.

Kisha kuna asili na kiasi cha taka, na kiasi cha joto kinachozalisha. Taka za kati hutoa joto kidogo na hivyo zinaweza kuhifadhiwa kwa usalama na kwa pamoja. Takataka za kiwango cha juu za nyuklia huzalisha joto zaidi, na lazima zihifadhiwe kwa kiasi kidogo, mbali mbali.

Pia kuna haja ya vizuizi kuzuia mionzi kutoka nje, ambavyo vinaweza kujumuisha vyombo vya kuhifadhia na miamba inayoizunguka.

Kuhakikisha usalama

Ujenzi wa mahandaki ya kuhifadhi taka za nyuklia kwa maelfu ya miaka - BBC News Swahili (4)

Chanzo cha picha, Tapani Karjanlahti/TVO

Wahandisi wa Ufaransa wameunda njia panda ya kilomita 4 (maili 2.5) ili kudhibiti usalama. Pia watatumia roboti kusogeza mitungi ya taka katika tukio lisilotarajiwa kama tetemeko la ardhi.

Nchini Sweden, mipango iko mbele zaidi. Kulingana na Anna Porelius, mkurugenzi wa mawasiliano wa SKB, shirika linalodhibiti taka za nyuklia za Sweden:

"Miaka ya 2080 hifadhi hiyo itajumuisha kilomita 60 (maili 37) ya mahandaki na nafasi ya zaidi ya matangi 6,000 ya shaba ya mafuta yaliyotumika ya nyuklia.”

Uwekaji wa taka za nyuklia utafanywa na mashine iliyoundwa maalumu ambayo inaweza kuendeshwa kwa mbali kwa usahihi mkubwa. Mashine itatumika kuweka mikebe ya shaba kwenye mashimo ya mita 500 (futi 1,650) chini kwenye mwamba.

Lakini teknolojia hubadilika. Kwa hivyo, lazima kutengeneze kituo kinachoweza kurekebishwa, kubadilishwa na kustahimili kwa muda mrefu.

Linapokuja suala la uhifadhi wa nyuklia, miradi hii itachukua mamia ya miaka kukamilika. Kwa hivyo ni nini kinachowapa motisha wataalamu hawa kufanya kazi kwenye mradi ambao hawatoshuhudia kukamilika kwake?

Porelius anasema, "hakuna hata mmoja wetu anayeweza kuona mradi wa hifadhi ya taka za nyuklia ukikamilika, lakini kile tunachofanya sasa ni suluhisho la taka za nyuklia kwa faida ya vizazi vijavyo. Kufanya hivyo... kunatupa motisha ya kusonga mbele."

Pia unaweza kusoma
  • Saa ya Siku za Mwisho za dunia iko sekunde 90 kabla ya janga

  • Marekani yaishuku Urusi kutengeneza silaha za nyukilia

  • Maangamizi ya nyuklia yanaweza kutokea, Mkuu wa Umoja wa mataifa aonya

Imetafisirwa na Rashid Abdallah na kuhaririwa na Ambia Hirsi

Ujenzi wa mahandaki ya kuhifadhi taka za nyuklia kwa maelfu ya miaka - BBC News Swahili (2024)
Top Articles
Latest Posts
Recommended Articles
Article information

Author: Van Hayes

Last Updated:

Views: 6354

Rating: 4.6 / 5 (66 voted)

Reviews: 89% of readers found this page helpful

Author information

Name: Van Hayes

Birthday: 1994-06-07

Address: 2004 Kling Rapid, New Destiny, MT 64658-2367

Phone: +512425013758

Job: National Farming Director

Hobby: Reading, Polo, Genealogy, amateur radio, Scouting, Stand-up comedy, Cryptography

Introduction: My name is Van Hayes, I am a thankful, friendly, smiling, calm, powerful, fine, enthusiastic person who loves writing and wants to share my knowledge and understanding with you.